MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri nchi
Kavu na Majini Mkoani Tanga (Sumatra) umewapa muda wa siku mbili wamiliki wa
mabasi mkoani hapa kuhakikisha wanahamia kwenye kituo kipya cha mabasi
kilichopo kange jijini Tanga ndani ya siku mbili zijazo la sivyo watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
Agizo la hilo lilitolewa na
Ofisa Mfawizi wa Sumatra Mkoa wa Tanga, Walukani Luhamba wakati alipofanya
ziara ya kutembea kituo hicho kuangali namna ya agizo la Mkuu wa mkoa wa Tanga,
Said Magalula namna linavyokwenda.
Alisema kuwa kimsingi wamiliki hao
kuendelea kubaki kwenye stendi ya zamani ikiwemo wengine kupaki magari
pembezoni mwa ofisi zao zilizopo karibu na maeneo hayo ni kukiuka amri
iliyotolewa na mamlaka hiyo hivyo watakaobainika kufanya hivyo baada ya muda
uliotolewa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha alisema licha ya kuchukuliwa
sheria kali kwa watakaobainika kukaidi agizo hilo lakini pia watawatoza faini
ya sh.lakini mbili (200,000) pamoja na kuvutiwa leseni ili kuweza kuwa fundisho
kwa wengine wenye tabia kama hizo.
Ofisa huyo alisema kuwa serikali
imetumia fedha nyingi kuhakikisha stendi hiyo inakuwa katika kiwango kizuri kwa
ajili ya kupunguza msongamano eneo la mjini kwa kuijenga lakini wao wameshindwa
kufikiria suala hilo na kuendelea kubaki mjini.
Awali akizungumza ,Mwenyekiti wa
Muungano wa Wasafirishaji wa Daladala
Jijini Tanga,Atwabi Shabani aliwataka wamiliki hao kuhakikisha
wanazingatia agizo hilo ili kuweza kuepukana na adhabu wanazoweza kukumbana
nazo.
Kwa upande wao baadhi ya madereva
wanaofanya safari zao kati ya Tanga na mikoa mengine waliotii agizo hilo
waitaka mamlaka hiyo kwa kushiriki Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama
barabarani kuhakikisha wanasimamia suala hilo ipasavyo ili kuepusha malalamiko.
Mmoja kati ya madereva hao,Omary
Chuchuli alisema kuwa utaratibu huo ni nzuro kwa sababu unaondoa manung;uniko
kwa baadhi ya wasafirishaji wengine ambao walikwisha kutii agizo la kuhamia
kwenye kituo hicho cha mabasi.
Naye Fadhili Jumanne alisema lazima
vyombo vinavyohusika na jambo hilo kuhakikisha vinashirikiana kwa pamoja ili
kuweza kuondoa changamoto hiyo iliyopo.
EmoticonEmoticon