“BELLE 9, PHD, IZZO B KUTUMBUIZA TANGA USIKU WA WAPENDANAO”

February 06, 2015
WASANII nguli wa mziki wa Bongo Fleva hapa nchini Belle 9,Hemed Phd na Izzo Business wanatarajiwa kutumbuiza katika onyesho maalumu la Red &White Party kwa wapendanao .
Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika February 14 mwaka huu kwenye ukumbi wa Club Lacasa Chika kuanzia saa saa tatu usiku mpaka majogoo ambapo wasanii hao watasindikiwa na wasanii wengine kutoka mkoani hapa.

Akizungumza na TANGA RAHA BLOG, Mratibu wa Onyesho hilo,Mbwana Imamu ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni  ya Arbarb Intertainment alisema kuwa maandalizi yake yamekamilika kwa asilimia kubwa na wasanii watakaotumbwiza watawasili mkoani hapa siku moja kabla.

 

 Mbwana alisema kuwa lengo kubwa la onyesho hilo ni kuwapa burudani wakazi wa Tanga hasa kwenye siku hiyo maalumu ya wapendanao ambayo huazimishwa kila mwaka hapa nchini.
   “Napenda kuwataka wakazi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi
kwenye onyesho hilo maana litakuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayofanyika “Alisema Mratibu huyo.

 
 Aidha aliwataja wasanii wa mkoani Tanga watakaosindikiza onyesho hilo kuwa ni Man Sasha, Kidani, Meratha, Voicer na Fat Zinga ambao watauwasha moto kwenye ukumbi huo siku hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »