Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bibi Joyce Fisoo( wakwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu filamu hiyo
iliyokuwa ikirekodiwa na raia wa Norway katika Ofisi ya Bodi ya Filamu
jijini Dar es Salaam
Raia wa Norway waliokamatwa wakiwa katika kikao kuhusu filamu waliyokuwa wakirekodi kwenye Ofisi ya Bodi ya Filamu.
Torshin Nodland raia wa Norway (watatu kulia) akijitetea kuhusu filamu hiyo waliyokuwa wakirekodi.
Baadhi ya vifaa walivyokuwa wakitumia raia hao wa Norway katika kurekodi filamu hiyo vikiwa katika Ofisi ya Bodi ya Filamu.
………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Raia watatu wa Norway wamejikuta
mikononi mwa Bodi ya Filamu nchini baada kuchukua picha kwa ajili ya
kutengeneza makala ya filamu inayohusu kazi za kutafsiri filamu za nje
zinazofanywa na Bwana Derick Mukandala maarufu kama Mzee Lufufu maeneo
ya Vingunguti.
Wageni hao hawakuwa na kibali cha kutengeneza filamu
kinachotolewa na Bodi hiyo hii ni kutokana na kunywimwa kibali kwa
makubaliono ya kubadili mswada wa filamu hiyo.Uongozi wa Bodi ya Filamu
iliwabaini zoezi hilo katika operesheni zake za kawaida zilizofanyika
mwishoni mwa wiki,.
Miongoni mwa wageni hao waliobainika ni mwandishi wa
Mwongozo/Mswada (Script) Bw.Bjorn_Eric Hansen, Mpiga Picha(Cameraman)
Bw.Torshin Nodland na mnasa sauti,kutoka Kampuni ya Grunder Film ya
nchini Norway.
Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Bibi Joyce Fissoo alisema filamu hiyo iliyokuwa ikitengenezwa na wageni
hao kwa kushirikiana na Kampuni ya Get Real Training ya hapa nchini
ilikuwa inahusu kazi anazozifanya Mzee Lufufu zinazokinzana na Sheria ya
Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya 1976 na pia Sheria ya Hakimiliki
na Hakishiriki ya mwaka 1999 ya nchi.
Bibi Fisoo aliendelea kusema bodi ya Filamu haiwezi kuruhusu
utengenezaji wa filamu hiyo inayoonyesha ukiukwaji wa Sheria kwani kuna
kinzana na juhudi za serikali katika kupambana na uharamia wa kazi za
filamu na kwamba kamati tayari ilikwisha waandikia wahusika barua ya
kuzuia uandaajwi wa filamu hiyo.
“Wajumbe wa kamati ya vibali walielekeza wahusika kubadili
maudhui ya mswada wao wakati walipopitia maombi ya kibali jambo ambalo
halikukamilishwa. Hii ni kwa sababu mswada wa kutengeneza filamu hiyo
unaonyesha kwamba mhusika watakayemtumia ni mtu ambaye amekuwa akikiuka
Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 1999,pamoja na mikataba ya
Kimataifa inayosimamia Hakimiliki na Hakishiriki kama vile Mkataba wa
Berne ambao Tanzania imeridhia ”,alisema Bibi Fissoo.
Kwa upande wa raia hao wa Norway walikiri kuvunja Sheria na
kukiuka taratibu za uandaaji wa filamu katika nchi na kuomba kwenda
kubadili mswada wa filamu hiyo kwa mara nyingine ili waweze kuwasilisha
upya pamoja na kufuata taratibu za kuomba kibali cha kutengeneza filamu
kwa mujibu wa Sheria za nchi na ithibati ya Hakimiliki kutoka COSOTA.
“Kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza
Na. 4 ya mwaka 1976, iwapo Bodi itadhihirisha ukiukwaji wa sheria hiyo
itaamuru tozo la faini papo kwa papo isiyopungua shillingi milioni moja,
kuamuru kusitisha utengenezaji wa picha jongevu husika au kuamuru
mkosaji kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria”alisema Bibi Fissoo.
Kwa niaba ya wenzake Bw.Hansen alisema wameipokea faini hiyo na
wanaahidi kulipa faini mara moja na kuwasilisha risiti, aidha walioomba
radhi kwa kosa hilo na kuahidi kutotumia picha hizo mahali yoyote.
Katika kuthibitisha raia hao wa Norway hawataendelea na zoezi la
uchukuaji wa filamu hiyo, Bodi ya Filamu iliwekaana makubaliano nao kwa
maandishi kuwa kutoendelea kupiga picha hizo hadi pale
watakapobadilishi muswada wao na kupewa kibali cha kutengeneza filamu.