SKYLIGHT YAENDELEA KUKONGA NYOYO MASHABIKI WAKE NDANI YA ESCAPE ONE MIKOCHENI NI KILA SIKU YA JUMAPILI

September 27, 2015

Wanaume wa shoka wakilisakata rhumba wakati wa kuwafurahisha mashabiki wa bendi ya Skylight wakati wa mkesha wa eid
Mwimbaji wa bendi ya Skylght Natasha akiwa anawapa mashabiki vionjo vya nyimbo za taratibu (kistaarabu) wakati wa mkesha huo wa Eid ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni
Bendi ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao huku mbele kabisa akiwa anawaongoza wenzake katika uimbaji wa nyimbo hiyo Sony Samba.
Ashura Kitenge (kushoto) akiwa na Kasongo Junior wa Skylight band wakitoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni
Sam Mapenzi ni muimbaji mashuhuri na huwa anajua kukonga nyoyo za watu hususani katika ule muziki wa Afrika magharibi weee utampenda hata kwa mkopo, hapo akiwa anaimba kwa kushirikiana na wenzake ndani ya bendi ya Skylight siku ya mkesha wa Eid.
Hii siku zote huwa inapatikana ndani ya Skylight tu na sio kwingineko maana ukihitaji kuburudika njoo tuungane pamoja katika bendi yetu inayoenda kwa kusikiliza mashabiki zaidi na sio kubagua mashabiki.
Mashabiki sasa zamu yao kulisakata wakati bendi ya Skylight ikiwa inatoa burudani hiyo ndani ya Escape One Mikocheni
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiwa katika hatua yake ya kukusanya mashabiki ili tu waende sawa aisee huyu jamaa ni hatari jumapili hii atakuwepo pale Escape One Mikocheni bila kukosa sogea taratibu uje ushuhudie vitu kutoka Skylight band.
Sam Mapenzi (kushoto) akiwa na Ashura Kitenge wakitoa burudani ya nguvu ndani ya Skylight band wakati wa mkesha wa kuamkia sikukuu ya Eid
 Mmoja wa viongozi wa Bendi ya Skylight Joshua Ndege (katikati) akionyesha umahiri wake sambamba na waimbaji wa bendi hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »