Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo
amepokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka katika taasisi
ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala
Uganda.
Pichani kiongozi wa Taasisi hiyo
Dkt.Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla
fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam Septemba 8, 2015 .
asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo Rais kikwete amepokea tuzo ya kuitambua
Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na
Utulivu,Huduma bora za jamii,na maendeleo makubwa ya kiuchumi katika
kipindi cha miaka kumi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akisaini kumbukumbu maalum ya taasisi ya East Africa Books of Records
mara baada ya kupokea tuzo maalum ya kiongozi bora Afrika mashariki kwa
kudumisha amani nchini na katika jumuiya ya
Afrika Mashariki kwa ujumla hususani Kenya baada ya uchaguzu mkuu na Burundi hivi karibuni.Kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Africa Book of Records Dkt.Paul Bamutize na kulia ni Mkuu wa kitengo cha utafiti katika taasisi hiyo Bwana Luzindana Adam Buyinza.
Afrika Mashariki kwa ujumla hususani Kenya baada ya uchaguzu mkuu na Burundi hivi karibuni.Kushoto akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Africa Book of Records Dkt.Paul Bamutize na kulia ni Mkuu wa kitengo cha utafiti katika taasisi hiyo Bwana Luzindana Adam Buyinza.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho akitoa hotuba yake baada ya kupokea Tuzo ya Kingozi bora Afrika Mashariki.
Mwakiulkishi kutoka ubalozi wa
Uganda nchini Tanzania Bwana Stephen Kiyingi akitoa hotuba yake na
ushuhuda jinsi Tanzania ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo katika miaka
kumi iliyopita.
Baadhi ya Wageni walihudhuria hafla hiyo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza mabalozi kutoka nchi za Afrika ya Mashariki muda mfupi baada ya kupokea Tuzo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete,Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, mabalozi kutoka nchi za
Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tassisi ya
East Africa Book of Records ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Wataalamu wa Utafiti kutoka
Taasisi ya East Africa Book Of Records wakiwa katika picha ya pamoja na
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada kutunikiwa Tuzo
hiyo.Kutoka kjushoto ni Kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul
Bamutize,Watatu kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utafili cha taasisi hiyo
Bwana Luzindana Adam Buyinza na kulia ni Afisa mwandamizi wa Taasisi
hiyo Bwana Kato Issa.
(Picha zote na Freddy Maro)