Maafisa,
Wakaguzi, na Askari wa Jeshi la Polisi hapa nchini, wametakiwa
kudunisha nidhamu wakati wote, kutenda haki kwa kila mmoja na
kuwaheshimu wananchi wa rika zote bila ya kujali dini, rangi ama itikadi
zao kisiasa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, SACP Ali Lugendo, wakati akizungumza na Wanafunzi wa Mafunzo ya Uofisa (Mrakibu Msaidiizi wa Polisi) na wale wa cheti na Stashahadi ya Sayansi ya Polisi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kamanda
Lugendo amesema kuwa pamoja na kufundisha masomo ya sheria na haki za
binadamu, lakini kazi kubwa inayofanywa na chuo chake ni kusisitiza
nidhamu kwa kila afisa na askari wanaofika chuoni hapo.
Amesema
kuwa nidhamu ni somo la kwanza analofundishwa askari anapokuwa katika
mafunzo ya awali kwenye chuo cha Polisi Moshi kwani amesema nidhamu ni
msingi wa kwanza kwa majeshi yote duniani.
“Hakuna
Jeshi lolote duniani, likiwemo Jeshi letu la Polisi hapa nchini ambalo
haliendeshi kwa misingi ya nidhamu”. Alisema Kamanda Lugendo na kuongeza
kuwa bila nidhamu hakuna Jjeshi.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Nidhamu kwenye chuo cha Polisi Dar es Salaam (Dar es Salaam Police Academy)
SSP Mussa Loyd, aliwataka Maafisa hao kuwa kioo cha jamii na kuwatendea
haki wananchi bila ya upendeleo wakati wote wanapokuwa kazini katika
maeneo mbalimbali.
Alisema
kuwa, mbali ya kuzuia vitendo vya kuhalifu, kushuku, kupeleleza na
kuwakamata watuhumiwa, lakini kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni
kuhakikisha kuwa kila Askari anatenda haki kwa kila anayemhudumia bila
ya ubaguzi ama kumuonea mmoja wao.
“tunachotakiwa
kufanya sisi Polisi ni kutenda haki kwa kila mmoja bila ya kujali dini,
kabila, rangi ama itikadi ya mwananchi kisiyasa maana sisi hatuna
chama”. Alisema Loyd.
EmoticonEmoticon