ACHANA
na mazingira ya kifo cha Bilionea maarufu wa Bukoba, Leonard Mtensa
aliyefariki saa chache baada ya kufanya mapenzi ndani ya gari kuacha
gumzo, gumzo lingine lilitokea wakati wa mazishi yake ambayo
yalihudhuriwa na wananchi wengi kutoka ndani na nje ya mkoa, mkanda
kamili huu hapa.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mazishi hayo mwanzo mwisho,
msiba huo ulikuwa wa pekee kwani haijawahi kutokea kwa yeyote kuzikwa na
umati mkubwa kiasi hicho na kusababisha watu wote wasimame kiasi cha
kuwafanya askari wa usalama barabarani kufanya kazi ya ziada kuhakikisha
mambo yanakwenda sawa.
“Ilikuwa si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi kutokea
msiba wa mtu wa kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani,
trafiki kuongoza harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo.
Inadaiwa kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari
mengine yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye
foleni nyumbani.
Jeneza likibebwa kuelekea makabulini.
Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani
kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho
kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari
yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini.
EmoticonEmoticon