Kongamano hilo la utoaji wa elimu kwa wauguzi hospitali na Zahanati Wilayani humo liliandaliwa na Chama cha Wauguzi Tanzania (TAMA) kwa ufadhili wa Shirika la Sanof Expour na kumshirikisha Muuguzi Mstaafu kutoka Canada kama anavyooneka hapa katikaipicha akiwa ameshikilia Camera.
Muuguzi Mkufunzi, Elizabert Mwakalinga akiangalia picha kwenye simu inayoonyesha madhara ya wazazi wanaojifungulia katika vituo ambayo sio vya kutolea huduma na hivyo wazazi kukumbana na changamoto nyingi zikiwemo za kupoteza watoto na mzazi
Elizabert Mwakalinga anaendelea kuishangaa picha hiyo ambayo ilikuwa ikihuzunisha na kuwashauri wanafunzi wauguzi katika darasa hilo kutoa elimu majumbani ili mzazi mjamzito kuwa na ada ya kuhudhuria vituo vya Afya.
Mkufunzi Muuguzi, Elizabert Mwakalinga akitoa somo katika darasa la Elimu kwa wauguzi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wauguzi Tanzania (TAMA)
Wauguzi kutoka vituo mbalimbali Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakifuatilia masomo, Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wauguzi Tanzania (TAMA)
Mratibu wa mafunzo hayo, Martha Rimoi alikuwa bega kwa bega na wakufunzi kuhakikisha kila kitu kinaenda vyema na hata pale alipokuwa na mchango hakuwa nyuma alikuwa akiongezea na kujibu maswali kwa washiriki kama anavyoonekana hapa kushoto alievaa miwani.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwa kushirikiana na mdau kutoka Canada pamoja na Shirika la SANOF
EmoticonEmoticon