WALIOWEZESHWA NA TBL KUPITIA PROMOSHENI YA SAFARI LAGER WEZESHWA WAPATA MAFANIKIO MAKUBWA

November 07, 2014

 Valerian Luzangi (kushoto) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo  ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.

 Valerian Luzangi (kulia) ambaye ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha shampoo za binadamu na wanyama hasa mbwa cha L & V Intergrated Firm akimuonesha Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi,  shampoo ya kuoshea mbwa ambayo iko tayari kuuzwa. Tbl kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa ilimpatia  mfanyabiashara huyo chupa 20,000 za kuwekea shampoo. Kiwanda hicho kipo Mikocheni Dar es Salaam.

 Mmoja wa wafanyakazi walioajiriwa na kiwanda hicho akiweka maji kwenye pipa tayari kuchanganywa na dawa wakati wa kutengeza shampuu.


 Mfanyakazi wa kiwanda hicho akiweka dawa kwa ajili ya kutengeza shampoo ya kuoshea nywere za binadamu

 Wafanyakazi wakibandika lebo kwenye chupa zenye shampoo

 Chupa zenye shampoo zikiwa tayari
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Leither Product, Jamhuri Oisso (kulia), akimuonesha Meneja Uhusiano wa TBL, Editha Mushi moja ya viatu wanavyotengeneza katika kiwanda cha kushona viatu kilichopo Manzese, Dar es Salaam kilichowezeshwa mashine na TBL,

 Baadhi ya viatu vinavyotengenezwa katika kiwanda hicho
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Leither Product, Jamhuri Oisso (kulia), akimuelekeza fundi  Amir Mbungi jinsi ya kushona viatu kwa kutumia cherehani cha kisasa katika karakana yake iliyopo Manzese, Dar es Salaaam. Cherehani hiyo alipewa tuzo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Leither Product, Jamhuri Oisso akionesha jinsi ya kutumia mashine za kisasa kubandika soli ya viatu katika karakana hiyo.mashine hiyo alipewa tuzo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Promosheni ya Safari Lager Wezeshwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »