LINNAH ATUMBUIZA KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI MKOANI TANGA.

November 07, 2014
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ,Linah Sanga jana alikuwa kivutio cha aina yake baada ya kuamua kujaza fomu za kujiunga na mfuko wa pesheni wa GEPF na kusababisha wanawake waliokuwa wamehudhuria mafunzo ya kampeni ya mwanamke na uchumi na kumfuata.

Linah ambaye pia ni balozi wa Angels Moment inayoendesha kampeni ya mwanamke na uchumi alijaza fomu za uanachama wa GEPF katika banda la maonesho lililowekwa Naivera Jijini Tanga yalikokuwa yakifanyika mafunzo  hayo.

Msanii huyo aliamua kujiunga na mfuko huo mara baada ya maafisa wa GEPF wakiongozwa na Meneja wa Mkoa wa Tanga,Silvanus Kuloshi kumweleza juu ya faida za uanachama wa mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa .

Nimeamua kujiunga na GEPF kwa sababu nimevutiwa na mafao yanayotolewa na natoa wito kwa wanawake wengine wakiwamo mashabiki wangu kujiunga nao”alisema Linah.

Kabla ya kuujiunga na mfuko huo,msanii huyo alikonga nyoyo za
madshabiki wake kwa kuimba nyimbo za kuwahamasisha wanawake kuendesha shughuli za ujasiliamali kwa kujiamini .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »