Na Maryam himid kidiko na Kijakazi Abdallah-Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itaendelea na juhudi zake za kuwaelimisha Wananchi ili waachane na tabia
ya kujenga karibu na maeneo ya Kambi za Kijeshi kwa lengo la kuepuka
usumbufu pamoja na madhara yanayoweza kuwakumba baadae.
Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi
Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Abuod wakati akijibu suala la
Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma katika kikao cha tano
kinachoendelea cha Baraza la Wawakilishi.
Saleh alitaka kujua kuwa lini
Serikali itafikiria kuzihamisha kambi za kijeshi zilizopo karibu na
Makaazi ya Raia na kuzipeleka nje ya Miji na Vijiji.
Waziri Aboud alifahamisha kuwa
katika nchi yoyote ile duniani kambi za kijeshi huwekwa Kimkakati kwa
lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi husika ikiwemo
Zanzibar.
Alisema Kambi zilizopo nchini sio
tatizo na kwamba zimewekwa kwa kuzingatia haja ya kiulinzi, usalama na
mazingira ya Zanzibar ilivyo.
Ameongeza kuwa Jeshi la Wananchi
linahitaji maeneo maalum yakiwemo ya kufanyia mazoezi ili kujiweka
tayari kwa adui yoyote Yule atakaeingia katika nchi kwa kufanya uadui.
Hata hivyo aliongeza kuwa kwa sasa
kambi zilizopo zilijegwa kwa miaka mingi iliyopita na kwa wakati huo
maeneo hayo hayakuwa karibu na makaazi ya raia.
Amesema kutokana na maeneo ya
Kambi hizo kuvamiwa na Wananchi kwa lengo la kuanzisha Makaazi limekuwa
tatizo na kwamba juhudi zinafanywa kuondokana na tatizo hilo ikiwemo
kuwaelimisha Wananchi juu ya Madhara yanayoweza kujitokeza
EmoticonEmoticon