,TANGA.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora,George Mkuchika amewaagiza maafisa Takukuru kwenye Halmashauri nchini kuhakikisha wanakwenda kukagua taarifa ya fedha za miradi ya maendeleo jinsi zilivyotumika kwenye maeneo yaliyokusudiwa ili kuweza kubaini hali halisi.
Hayo aliyasema jana wakati akizungumza kwenye kikao cha Ushauri wa Mkoa wa Tanga (RCC) ambapo alisema kuwa miradi mingi kwenye halmashauri hapa nchini imegauzwa kuwa sehemu za kuchukulia fedha kwa watumishi wasiokuwa waaminifu jambo ambalo linakwamisha shughuli za maendeleo.
Alisema kuwa jambo hilo linatokana na wasimamizi wakuu wa halmashauri wakiwemo wakurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wanachangia kwa asilimia kubwa kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo inayoendeshwa kwenye maeneo yao hali inayopelekea kujengwa chini ya kiwango na kushindwa kudumu kwa muda mrefu.
“Kwenye suala hili hakuna jinsi lazima maafisa Takukuru kwenye
halmashauri kuacha kukaa ofisini badala yake mhakikisha mnakwenda kuziangalia fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yenu kubaini mambo yanayokwenda nah ii itasaidia uwajibikaji kwa wahusika “Alisema Mkuchika.
Alisema kuwa ili kuweza kuhakikisha jambo hilo linamalizika kwenye maeneo husika lazima kuwepo kwa watendaji waadilifu ambao wataweza kuzingatia maadili hasa kwenye miradi inayotekelezwa na serikali hali itakayosaidia kuondona na vitendo vya rushwa kwenye maeneo husika.
Akizungumzia takwimu za hali ya rushwa kwenye mkoa wa Tanga,Waziri Mkuchika alisema kuwa mkoa wa Tanga una tuhuma 192 za rushwa zilizoripotiwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai mwaka jana hadi kufikia mwaka huu jambo ambalo linatokana na kutokuwa na watumishi wasio waadilifu.
Aliitaja maeneo ambayo yamekithiri kutokana na rushwa mkoani hapa ni serikali za mitaa tuhuma 85,Idara ya afya na ardhi ambazo
waliokamatwa na rushwa walikuwa ni 19,Polisi ni 15,Sekta binafsi
3,Mahakamani 10,Elimu 10,Ujenzi 5 na Mamlaka ya Mapato mkoa wa Tanga(TRA) zilizokuwa ni 5.
Alisema kukithiri kwa rushwa kwenye maeneo mengi hapa nchini ikiwemo kwenye halmashauri inatokana na watendaji pamoja na viongozi kushindwa kizitumia kamati za maadili za uongozi ili kuweza kuongeza utawala bora badala yake wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwa na kamati ambazo zinaweza kuwaingizia posho.
Hata hivyo alizitaka idara ambazo zimekuwa kabiliwa na tuhuma za
rushwa kuhakikisha wanatafuta mbinu na mikakati ya kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hilo kwenye maeneo yao ili kuhakikisha rushwa inakomeshwa kabisa katika maeneo yao.

EmoticonEmoticon