Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika-
Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa
nyuma yake ni Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika-
Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika-
Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi namba 1 la nchi za
Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
…………………………………………………………
Na Ingiahedi Mduma-Washington D.C
Mkutano wa kundi namba 1 la nchi
za Afrika hufanyika kila mwaka wakati wa mikutani ya Benki ya Dunia na
IMF na unahusisha kundi la nchi za Benki ya Dunia ambazo zinapata mikopo
nafuu kutoka IDA. IDA ni shirika au mfuko wa maendeleo kwa ajili ya
kutoa mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia.
Katika mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za
kibenki na mambo ya utawala kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa
mikutano hiyo na kamati mbalimbali. Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri
wa Fedha. Kwa mwaka 2014 -16 Mwenyekiti atakuwa Waziri wa Fedha kutoka
Ethiopia na Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi hawa wataongoza mpaka
mwaka 2016. Mwaziri wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni MaGavana
mbadala, hivi ni vyeo vya uwakilishi kattika Benki ya Dunia.
Akiongea katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake
alisema kuwa”tumepata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza la
nchi za Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake
anatoka Zimbabwe “ alisema.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa
anayemaliza muda wake anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa
wanachaguliwa kwa kupigiwa kura na kila nchi. “Hawa watakuwa watendaji
moja kwa moja kuanzia sasa na nafasi hizi zinapatikana kwa
mzunguko.”alisisitiza..
Vilevile katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo
ambayo itakuwa na mwenyekiti ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka
Tanzania, Namibia pamoja na Sierralion.
Jambo lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni
kwamba Benki itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea
toka kwenye mfuko wa IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika.
Vilevile walisisistiza suala la gonjwa la EBOLA. Walielezea kuwa
wataendelea kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo
tatizo.
Pia Benki ya Dunia itaendelea kupeleka wafanyakazi kujifunza
jinsi Benki ya Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu
kuchagua watu wazuri ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze
kutumia ujuzi wanao upata.
Mwisho walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia
jitihada ambazo zinalenga matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya
kazi kwa kuzingatia matwakwa ya BRN. Hivyo wanatagemea fedha
zinazotolewa zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa sasa.
EmoticonEmoticon