JESHI
la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya
ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na
kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri.Akizungumza
Dar es Salaam, Septemba 3,2014 Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema
kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani
kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.
“Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya
watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kinyume na malengo
yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi, kashfa,kuchafua
viongozi wa Serikali.
“Wengine wamekuwa wanasambaza
picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina, ingawaje
mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria
haitamuacha, alisema.
Senso aliendelea kubainisha kuwa
kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu ya kuepuka
kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila
kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.
Alisema oparesheni ya kuwabaini
wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina
hiyo.
Aliongeza kuwa hatua hiyo pia
inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya utapeli na
kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs
zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.
“Wapo baadhi ya watu wanatumia
mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu
ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa hatua
kali zitachukuliwa dhidi yake,” alisema.
Hivyo alisisitiza kuwa Jeshi hilo
linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu huo, na kuwataka wale
wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali waufute.
Pia aliziomba kampuni za simu za
mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina hiyo wasiruhusu uende kwa
mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na uovu huo.
EmoticonEmoticon