SILVER ATAKA KAZI ZA WASANII ZILINDWE.

September 03, 2014
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MSANII wa mziki wa Bongofleva mkoani Tanga,Sophia Patrick
“Silver”ameitaka wizara ya Habari Utamaduni na Michezo iweke sheria kali zitakazowezesha kulindwa kwa kazi zai ili wasanii wa mziki huo kupata mafanikio kutokana na kazi hizo.

Silver alitoa ushauri huo wakati akizungumza na Blog hii

ambapo alisema kuwa wasanii wamekuwa wakifanya kazi ngumu sana lakini mafanikio yanakuwa ni madogo sana kutokana na kuwepo kwa mianya ya kutokulindwa kazi hizo.

Alisema kuwa wakati umefika kwa mamlaka hizo husika kuhakikisha
  wanalivalia nyuga suala hilo kwa kuweka mpango kabambe ambao utawezesha kuondoa tatizo hilo hasa kwa wasanii chipukizi hapa nchini.

Akizungumzia changamoto ambazo wanakumbana nazo,Silver ambaye pia ni
  mwanafunzi wa Chuo Kikuu mkoani hapa akichukua masomo ya sanaa, alisema kuwa changamoto kubwa ni upande wa vyombo vya habari hususani watangazaji na madj ambao wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwao jambo ambalo lisipochukuliwa hatua huenda mziki huu ukatoweka .
Hata hivyo aliwataka wasanii wengine chipukizi kuhakikisha wanafanya  kazi zao kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kufikia malengo ya kuhakikisha wanautangaza vilivyo mziki huo ndani na nje ya nchi.

Msanii huyo hivi sasa anatamba na nyimbo zake mbili ambazo ni

“Univeristy  na Ingara ambazo ameziimba katika mahadhi tofauti tofauti chini ya Mtayarishaji wa mziki huo mkoani hapa Danny Toucher kupitia studio za Akili Music.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »