Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mechi ya leo. (Picha na Frank Momanyi)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MBRAZIL Geilson Santos Santana ‘Jaja’ kwa mara ya
kwanza akicheza katika uwanja wa kisasa wa Taifa jijini Dar es salaam
amefanikiwa kuifungia Yanga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Thika
United ya Kenya.
Katika mechi hii iliyoanza saa 11:00 jioni, Jaja
aliandika bao hilo katika dakika ya 60 ya mchezo.
Jaja ameweza kumfunika Mbrazil mwenzake, Andrey Coutinho
aliyoonekana kuwa moto wa kuotea mbali katika mechi tatu zilizopita.
Coutinho aliifungia Yanga mabao 2 katika mechi
tatu alizocheza Zanzibar wakati Jaja alifunga moja dhidi ya Chipukizi FC uwanja
wa Gombani Pemba.
Cuutinho aliitungua Shangani na KMKM, Yanga ikishindi
mabao 2-0 kwa kila mechi.
Lakini leo Jaja alitulia na kumzidi kete Coutinho
aliyetarajia kuwavutia mashabiki wengi wa Yanga.
Maximo aliwaanzisha pamoja Jaja, Saimon Msuva na
Coutinho katika safu ya ushambuliaji, wakati Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite
walianza katikati.
Winga ya kulia alianza Hassan Dilunga. Safu ya
ulinzi walianza Juma Abdul, kulia, Oscar Joshua, kushoto na mabeki wa kati
walianza Nadir Haroub na Kelvin Yondani.
EmoticonEmoticon