Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga akimtambulisha Mkurugenzi wa Kampuni ya S&D Collection
iliyotangaza udhamini wa shindano la Miss Tanzania Bi. Devotha Kajogoo
Mtambo kulia wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye
hotli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya S&D Collection
Bi. Devotha Kajogoo Mtambo akisisitiza wakati wa mkutano na waandishi
wa habari uliofanyika kwenye hotli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na
kulia ni Bi.Esther Maro Mkurugemzi wa S&D Collection
…………………………………………………………….
Na Majuto Omary
Kampuni
ya S &D collection kwa upande wa Boutique imetangaza udhamini wa
nguo kwa warembo wote 30 watakao wania taji la Miss Tanzania 2014
watakaopambana mwezi Oktoba jijini.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jumatatu, mkurugenzi wa S&D Collection,
Devota Kijogoo Mtambo alisema kuwa hatua ya kudhamini mashindano hayo ni
kujihusisha katika shughuli za kijamii mbali ya kujitangaza kupitia
jukwaa hilo.
Devota
alisema kuwa warembo wote 30 watazawadiwa nguo kuanzia shoo ya
ufunguzi, vazi la ubunifu, ufukweni na warembo watano watakaoingia
katika hatua ya fainali. Alisema kuwa pia watadhamini nguo za mshindi wa
taji la Miss Tanzania ambaye ataiwakilisha nchi katika mashindano ya
mwakani ya kumsaka mrembo wa dunia.
“Lengo
letu ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Kampuni ya Lino
International Agency ya kuendeleza mashindano ya urembo hapa nchini, ni
mashindano makubwa na ndiyo maana sisi tumeingia kutokana na ubora wake
na ubora wa bidhaa zetu,” alisema Devota.
Alisema kuwa kampuni yao itatumia si chini Dola za Kimarekani 27,000 (zaidi ya Sh Milioni 44) kwa ajili ya nguo za warembo hao.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency, Hashim Lundenga aliipongeza kampuni hiyo
kwa kudhamini mashindano hayo na wameikubali kutokana na uwekezaji wake
katika shughuli hiyo.
“Mashindano
yetu ni makubwa, kampuni ya S&D Collection ni kubwa na imewekeza
vilivyo katika mashindano yetu, hii itasaidia kuongeza ubora huku
warembo wakipata hafueni kwani hawataingia katika gharama za mavazi,”
alisema Lundenga.
Alisema
kuwa kwa sasa wanaendelea na mashindano ya Kanda kabla ya kuanza
maandalizi ya kambi ya Taifa mara baada ya kukamilika kupatikana kwa
warembo wote 30.
EmoticonEmoticon