Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto)
akiwakaribisha viongozi wa KAAT walipokwenda kumtembelea na kufanya nae
mazungumzo nyumbani kwake. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen
Katemba na Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT
(Zanzibar).
Rais
Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) akiongea na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) wakati walipokwenda
kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
Kulia ni Bw. Bukheti Juma ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar).
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akifurahia
jambo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Bukheti
Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya nae
mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
Bw.
Bukheti Juma (Kulia) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar) akiongea
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto)
wakati walipokwenda kumtembelea na kufanya nae mazungumzo nyumbani kwake
mjini Zanzibar. Katikati ni Rais Mpya wa KAAT, Bw. Stephen Katemba
akiwasikiliza.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Kushoto) akitilia
mkazo umuhimu wa jamii kusaidia wazee wasiojiweza, wakati alipofanya
mazungumzo na viongozi wa KAAT, Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw.
Bukheti Juma (Kulia). Viongozi hao walipokwenda kumtembelea na kufanya
nae mazungumzo nyumbani kwake mjini Zanzibar.
Baadhi
ya wanachama wa KAAT wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (Katikati).
………………………………………………………………………….
Na Saidi Mkabakuli
*Yadhamiria kuwasaidia wazee wasiojiweza
Uongozi mpya wa Jumuiya ya
Watanzania waliosoma Korea (KAAT) wamekutana na kufanya mazungumzo na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Zanzibar
na kutoa ombi rasmi la kuharakishwa kwa kufunguliwa kwa Ofisi za
Kibalozi nchini Korea Kusini.
Wakizungumza mara baada ya
kukaribishwa na Mhe. Balozi Iddi, Rais wa KAAT, Bw. Stephen Katemba
alitoa wito kwa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kufikiria
kufungua ubalozi nchi Korea Kusini kwa kuzingatia umuhimu wa nchi hiyo
katika uchumi wa Tanzania.
Bw. Katemba alisema kuwa
kufunguliwa kwa ubalozi huo kutaongeza chachu ya mahusiano ya kibiashara
na kindugu baina ya nchi hizi mbili zenye urafiki wa hali ya juu.
“Tunakosa fursa nyingi za kufanya
biashara na Korea Kusini kwani wengi wa wafanyabiashara wa Korea Kusini
tuliokutana nao nchini humo wanaona usumbufu kufuata huduma za kibalozi
nje ya nchi yao,” alisema Bw. Katemba.
Kwa mujibu wa Bw. Katemba, Korea
Kusini ina soko kubwa kwa bidhaa za Tanzania ikiwemo bidhaa za vyakula
na matunda, pia Tanzania ina fursa kubwa ya kupata ujuzi hasa kwenye
eneo la kiteknolojia na ujenzi.
Kwa upande wake Balozi Iddi,
alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu na fursa zilizopo nchini Korea,
na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo.
Wakati huo huo, katika kutimiza
wajibu wa kusaidia wazee na watu wasiojiweza, uongozi mpya wa Jumuiya ya
Watanzania waliosoma Korea (KAAT) upo mbioni kufanyia matengenezo
nyumba za kukaa wazee za Sebuleni, mjini Zanzibar.
Akizungumzia mpango huo, Makamu wa
Rais, KAAT (Zanzibar), Bw. Bukheti Juma amesema “KAAT inatambua mchango
mkubwa wa wazee nchini Tanzania, hivyo katika kuhakikisha wanaishi
katika mazingira safi na salama, KAAT tutafanyia matengenezo baadhi ya
majengo yaliyo kwenye hali mbaya kituoni hapo,” alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Juma zoezi hilo linatarajiwa kufanywa katikati ya mwezi ujao.
EmoticonEmoticon