TIMU ya Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kundoka mkoani hapa Jumanne
kuelekea Kisiwani Pemba kwa ajili ya kuweka kambi ya Mazoezi ya kujiandaa na
msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumza na Tanga Raha Blog leo katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema
kuwa kambi hiyo itawekwa visiwani humo mahali pamoja na kufanyia mazoezi kwa
timu hiyo kwenye uwanja wa Migombani kila siku.
El Siagi alisema kuwa kikosi cha wachezaji wapatao 25 ikiwemo Benchi la
Ufundi litakuwa na watu watano ambao wataelekea visiwani humo wakiwa na lengo
la kukisuka kikosi hicho kwa ajili ya kuleta ushindani msimu ujao.
Alisema katika benchi la ufundi litakuwa na Kocha mkuu Yusuph Chipoo,Kocha
Msaidizi Benard Mwalala na Kocha wa makipa Razack Siwa,Daktari wa timu pamaoja
na Kiti meneja.
Aidha alisema msafara wa timu hiyo utaondoka mapema mkoani hapa siku hiyo
kwa ajili ya kwenda kuanza kambi mpya ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa
Ligi kuu Tanzania bara.
EmoticonEmoticon