tar 11/5/2014 ambapo ni siku ya Mama Duniani, Mkurugenzi Mtendaji
ametembelea hospital tatu za jijini Dar es Salaam ili kuwafariji na
kuwapa moyo wazazi "Wakina-Mama" na kuwazawadia sabuni za kufulia.
Ziara ilianzia Temeke Hospital akiwepo Mkurugenzi Mtendaji, Katibu
John Tall na mpiga picha Rodgers na kuanza katika wodi ya Wazazi na
tulipokelewa na Shamim Kanju na tulipewa data kuwa jumla ya watoto 32 walizaliwa toka saa 6 usiku mpaka asubuhi ya leo ikiwa 13 Wanawake na 19 Wanaume.
Tukafika Ilala hospitali ya Amana nako tukapokelewa na Getrude Massawe na kupewa data watoto 94 walizaliwa ikiwa 44 Wanawake na 50 Wanaume na ziara yetu ikaishia Mwananyamala Hospital na tukapokelewa na Tuswege Mwamwanja na hapo pia tuka tembelea wodi ya wazazi na kupewa
data kuwa watoto 28 wamezaliwa ikiwa ni 12 Wanawake na 16 Wanaume.
hii inaleta jumla ya watoto 154 waliozaliwa kutoka saa 6 usiku mpaka saa 1 asubuhi "Wanawake 69 na Wanaume 85"
Kwa kweli mimi kama Mkurugenzi Mtendaji nikiwa na timu yangu tunapenda kutoa shukran zetu za dhati kwa uongozi wote wa Hospital tulizotembelea na kile kidogo tulichokuwa nacho tumeweza gawana na Wazizi tuliowafikia kama picha zinavyojieleza.
tunaiomba jamii kutupia jicho kwa Wanawake kwani tukiwezeshwa tunaweza... kwa habari na mawasiliano pitia www.wanawaketunaweza.com
EmoticonEmoticon