Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea
kwa masikitiko kifo cha Balozi wa Malawi nchini, Flossie Gomile-Chidyaonga
kilichotokea juzi (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Balozi
Gomile-Chidyaonga ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini
Tanzania mwaka 2011, alikuwa Naibu Balozi wa nchi hiyo Uingereza alifikwa na
mauti baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Msiba
huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Balozi
Gomile-Chidyaonga ndiye aliyefanikisha ujio wa timu ya Taifa ya Malawi (The
Flames) ambayo Mei 4 mwaka huu ilicheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars jijini
Mbeya.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Balozi Gomile-Chidyaonga, Ubalozi wa
Malawi nchini na Chama cha Mpira wa Miguu Malawi (FAM), na kuwataka kuwa na
subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
EmoticonEmoticon