Uncategories
NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYANI NZEGA, AFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Mbunge wa
jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala wakishiriki katika ujenzi wa jengo
la mapokezi OPD la hospitali ya wilaya ya Nzega wakati katibu mkuu huyo
alipokagua ujenzi wa jengo hilo leo katika ziara yake anayoendelea nayo
yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali
inayoshirikisha pia wananchi, pamoja na kusikiliza kero mbalimbali
zinazowakabili wananchi na kuzipatia au kuzitafutia majawabu, Ndugu
Abdulrahman Kinana pia anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa,
Itikadi na Uenezi katika ziara hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-NZEGA-TABORA)
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nzega leo jioni.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akielekeza jambo wakati
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa jengo
la OPD katika hospitali ya wilaya ya Nzega, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Tabora Mh. Fatma Mwassa.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Nzega leo jioni.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Fatma Mwassa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Nzega.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi
wa ofisi ya tawi ya CCM katika kata ya Nkiniziwa wilayani Nzega leo.
Ujenzi wa jengo la Hospitali ya wilaya ya Nzega ukiendelea.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akichangisha
fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofizi ya CCM kata ya Nkiniziwa, kulia ni
mbunge wa jimbo la Nzega Mh. Khamis Kigwangala akipokea michango
mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakimsikiliza mwanafunzi
wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Kampala Amos Kashindye, mara
baada ya kuitembelea shule hiyo na kukagua maabara ya sayansi na fizikia
katika shule hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili katika mji wa Ndala.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua vikundi vya ngoma.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua moja ya
barabara zinazojengwa mjini Nzega kwa kiwango cha lami, kushoto kwake
ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Mh.
Fatma Mwasa Mkuu wa mkoa wa Tabora.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza moja
wa wachimbaji wadogowadogo wa madini kutoka wilayani Nzega Samson Mabula
wakati alipotoa malalamiko kwa niaba ya wachimabji wenzake.
Mh. Khamis Kigwangala mbunge wa jimbo la Nzega akiwahutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Nzega leo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza mjumbe
wa mkutano mkuu wa CCM ndugu Hussein Bashe mara baada ya kukabidhi kwwa
viongozi wa kata pikipiki kwa ajili ya watendaji wa chama cha
Mapinduzi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon