April 07, 2014

YANGA YAIBANJUA JKT RUVU MABAO 5-1 UWANJA WA TAIFA

 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akiruka kukwepa kwanja la beki wa JKT Ruvu, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1. Mabao matatu yalifungwa na Mrisho Ngassa, katika dakika ya 7, Dakika ya 15 na Dakika ya 48. 

Mabao mengine yalifungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 39 na bao la tano likafungwa na Hussein Javu katika dakika ya 51.  Kwa ushindi huo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 49 wakiwa nyumba ya Azam Fc wenye jumla ya Pointi 53 kwa tofauti ya 4. Bao la kufutia machozi la JKT Ruvu lilifungwa na Nashon Naftari, katika dakika ya 83.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja kati ya mabao matano yaliyofungwa katika mchezo huo leo.
 Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
 Didier Kavumbagu (kulia) akichanja mbuga kumtoka mchezaji wa JKT Ruvu.
Kipa wa JKT Ruvu, akijaribu kuokoa moja kati ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »