BRAC TANGA YAONYA RUSHWA KWA WATENDAJI WAKE

January 14, 2014
TAASISI inayotoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo mkoani Tanga,(BRAC) imewaonya wafanyakazi wake kuacha tabia ya kuchukua rushwa kutoka kwa wanachama wanaoomba mikopo kwenye taasisi hiyo.
 

Meneja wa Mkoa wa Tanga wa Taasisi ya BRAC,Prodip  Laskar aliyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea ofisini kwake ambapo alisema tuhuma zozote za rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wake zitafuatiliwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria.


Kauli hiyo ya Meneja inatokanana na Taarifa zilizozagaa mkoani Tanga kuwa baadhi ya matawi ya Taasisi hiyo yanajihusisha na upokeaji wa rushwa kutoka kwa wateja wao hasa pindi wanapokuwa wakihitaji kupatiwa mikopo.


Alisema ofisi yake haijiusishi na suala hilo ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawapunguza wafanyakazi wote ambao wanajihusisha na vitendo hivyo kwani vitaweza kulichafulia jina taasisi hiyo.


      “Sisi kama taasisi tumejiwekea utaratibu wa kupambana na rushwa katika eneo letu la kazi na hasa ukizingatia tayari tumeshachukua hatua stahiki ikiwemo kuwafukuza kazi wafanyakazi watatu ambao walibainika kupokea rushwa “Alisema Laskar.
 

Hata hivyo aliongeza kuwa wataendelea kuweka utaratibu mzuri wa
kuwapatia mikopo wajasiriamali wadogo wadogo bila kuwepo na adha ya aina yoyote ile lengo likiwa kujikwamua na umaskini pamoja na kuongeza pato lao.
 

Taasisi hiyo tayari imekwisha kutoa mikopo kwa wajasiriamali mikopo yenye thamani ya sh.milioni 300 kwa walengwa wapatoa 10500 lengo likiwa la kuinua na kuboresha hali ya maisha ya wananchi

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »