HANDENI WAPITISHA BAJETI YA MWAKA 2014-2015

January 14, 2014
HALMASHAURI ya Mji wa Handeni, imepitisha mapendekezo ya bajeti yake ya mwaka 2014-2015 ya jumla ya kiasi cha sh. bilioni 7.9 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo fedha za utawala kwa watendaji.
Akisoma mapendekezo hayo katika baraza la madiwani la halmashauri ya mji huo mwishoni wa wiki, Kaimu Mwekahazina wa mji huo, Npella Kwidika amesema mapendekezo ya bajeti hiyo imezingatia mipango, sera na ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 na kwamba wamelenga kupata fedha hizo kwenye vyanzo vyao vya mapato na ruzuku toka Serikali Kuu.


Amesema makusanyo ya ndani wamepanga kukusanya kiasi cha sh. milioni 720 fedha zitakazolipa mishahara kwa watumishi ni sh. bilioni 5.9 ruzuku na matuminzi sh. milioni 709 huku miradi ya maendeleo wakiwa wamepanga kutumia kiasi cha sh. milioni 503.

Mwekahazina huyo pia amesema kwamba nje ya bajeti hiyo, wameomba hazina kiasi cha sh.bilioni  2.3 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala ambalo litagharimu kiasi cha sh. bilioni 1.5 fedha za kujenga maabara za shule za sekondari zipatazo nane zilizopo katika halmashauri hiyo kiasi cha sh. milioni 624 huku wakipanga kiasi cha sh. milioni 250 kwa ajili ya magari ya mkurugenzi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Thomas Mzinga amesema kwenye kikao hicho kwamba wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi milioni 200 kutoka katika kodi ya majengo katika mji huo utaratibu ambao unatarajiwa kuanza januari 15 mwaka huu na kwamba wananchi wote wametakiwa kulipa fedha hizo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »