DULLAH WA MICHANO:TUMEPANIA KUENDELEZA MZIKI WA BONGO FLEVA MKOANI TANGA.

January 05, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva Mkoani Tanga,Ally Khamisi "Dullah wa Michano"apania kuendelea mziki wa kizazi kipya mkoani hapa kwa kuwakutanisha wasanii hao lengo likiwa kuinua vipaji vyao.

Dulla wa Michano (Pichani Juu)alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na TANGA RAHA ambapo alisema bila jitihada na sapoti kubwa kwa wasanii ikiwemo kushirikiana mziki huo hauwezi kufika mbali hivyo lazima wasanii wakubali kuwa na mshikamano ili kuweza kuleta mapinduzi katika tasnia hiyo.


Michano ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake  "NAZEEKA"aliomshirikisha  kaka yake SELLE wa MICHANO amsema ana matumaini makubwa utafanya vizuri kama nyengine zilizopita ambavyo pia zinaendelea kuubamba mziki wa bongo fleva hapa nchini.

Wimbo huo aliurekodia kwenye studio za DIVA TALENT inayomilikiwa na MESEN SELECTA ambapo ni miongoni mwa nyimbo ambazo zimemtambulisha sana kwenye mziki huo ambao umeonekana kuwa na wapenzi wengi hapa nchini.

Akizungumzia mziki huo,alisema mziki wa bongofleva unalipa kilichobakia ni watu kuwa makini na kujitambua wanapaswa kufanya nini ili kuweza kuendana na ushindani.

 "Kama unavyojua mziki wa sasa unalipa tofauti na miaka ya nyuma hivyo wasanii wanapaswa kutumia umakini mkubwa hasa wakati wanapokuwa wakitunga mashairi yao na sio kukurupuka kitendo ambacho kinawapeleka kushuka badala ya kupiga hatua za kimaendeleo "Alisema Dulla wa Michano.

Aidha aliwataka watangazaji na watayarishaji wa mziki huo kuwapa nafasi wasanii wachanga ili nao waweze kuonyesha vipaji vyao badala ya kuwabania kwani kufanya hivyo kunapeleka kushuka mziki huo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »