DC DENDEGO AONGOZA BONANZA LA KUKUZA VIPAJI JIJINI TANGA.

January 05, 2014
 Na Burhan Yakub,Tanga.
Vijana wa mjini hapa jumamosi walionyesha vipaji vyao vya uchezaji michezo mbalimbali, uimbaji ,uchezaji muziki na kuendesha
pikipiki katika bonanza la kukuza vipaji lililofanyika katika uwanja wa shule ya msingi  Majani Mapana Jijini Tanga.

Bonanza hilo lililoratibiwa na diwani wa kaya ya Nguvumali,Selebosi Mustafa ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima
Dendego lilifanyika kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ambalo kwa mujibu wa melezo ya Selebos itakuwa ikifanyika kila jumamosi kwa kipindi cha miezi sita mfulizo ilikuwa ni soka ambayo zilichezwa mara tano,netboli nne,mchezo wa wavu mara tatu,kuvuta kamba wanawake na wanaume na kufukuza kuku.

Michezo mingine iliyofayika katika bonanza hilo ni mbio za pikipiki, kuonyesha vipaji vya uimbaji,uchezaji muziki na uigizaji.

Akizungumza katika bonanza hilo,Dendego alitoa wito kwa vijana kuhuduria kila jumamosi kwa sababu mbali ya kuonyesha vipaji pia inawaepusha na mambo maovu ambayo wangeyafanya mitaani.

Alisema pia bonanza hilo litatumika kuwakopesha vijana pikipiki kwa utaratibu wa kulipia sh 500,000 za awali na nyingine kuwasilisha taratibu.

Katika bonanza hilo,Afisa miradi wa kampuni inayojihusisha utoaji wa elimu ya ujasiliamali TZ8,Hamis Tembo aliwataka vijana kujenga tabia
yakuthubutu ili kujiletea maendeleo.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »