REA KUPELEKA UMEME WILAYA SITA MKOANI TANGA.

January 02, 2014
Na Oscar Assenga,Tanga.

WAKALA wa nishati ya Umeme Vijijini (REA)unatarajiwa kukamilisha miradi ya Umeme katika vijiji mbalimbali mkoani Tanga ambapo ikikamilika itaongeza huduma  hiyo kwa wananchi na wawekezaji waliopo kwenye maeneo yao hali ambayo itachangia kasi maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa aliyasema hayo juzi wakati akitoa taarifa ya mafanikio kwa mkoa wa Tanga kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2012 hadi Octoba 2013 ambapo alisema kwenye mpango  huo jumla ya wilaya sita zitanufaika.

Gallawa alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013-2014 wakala umepanga kupeleka umeme katika maeneo ya wilaya ya Handeni kwenye vijiji vya Kideleko,Kigombe, Madebe,Nyasa na Gole ili kuwawezesha wananchi hao kufaidika na huduma ya nishati.

Alisema kwenye wilaya ya Korogwe mji wakala wa nishati ya umeme vijiji watapeleka kwenye maeneo ya Maili Kumi,Taasisi ya Utafiti ya Tafori,Kwamgwe, Jambe,Kamsisi, Kwamndolwa, Kwakombo,Kwameta, Kwange,Msambiazi, Darajani,Gereza, Kwamzindawa,Mgobe, Kituo cha Afya Kwalukonge,Miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji ya Kitivo na Mombo.


 Mkuu huyo wa mkoa alisema katika wilaya ya Lushoto vijiji ambavyo vitanufaika na mradi huo ni eneo la Mlola kupitia vijiji vya Mnadani,Mtumbi,Mshangai,Kwekanga na Mathego wakati wilaya ya Mkinga watapeleka umeme vijiji vya Manza Bay,Daluni na Gombero.

Aidha aliitaja eneo lengine ambalo litafaidika na huduma hiyo ni Korogwe Vijijini ambapo wakala atapelekea nishati hiyo kwenye vijiji vya Malibwi, Manolo, Hambogo, Ngwelo,Dindira, Kijungumoto,  Kijango,Lusanga,Kwamazandu ,Makumba, Mkwakwani,Vugiri,Makose,Nkalai,Sunga,Kihitu,Malindi na Rangwi.

Katika wilaya ya Pangani wakala watapeleka umeme katika vijiji viwili ambavyo ni Mkalamo na Mbulizaga ambapo ukamilikaji wa miradi hiyo utasaidia wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo kupata nishati hiyo bila kikwazo.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »