Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha
Chiola, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya Mwenge huo kumaliza
kukimbizwa katika Wilaya Ruangwa. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu
2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze
Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya
Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na
kuzinduliwa. Picha zote na Felix Mwagara.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge
Mwaka 2014, Rachel Kassanda baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru
uliotoka Wilaya ya Ruangwa na kuingia Wilaya ya Nachingwea. Wapili
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo ambaye ndio
aliyekabidhiwa rasmi Mwenge huo kutoka Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Picha na Felix Mwagara.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (kulia) akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Chiola (hawapo pichani) baada ya kufungua Mradi
wa Nyumba ya Mganga katika Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru
ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya
Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa
katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo
itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Picha na Felix Mwagara.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (aliyebeba ndoo ya maji)
akishangiliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya
ya Nachingwea, Regina Chonjo pamoja na wananchi baada ya kubeba ndoo ya
maji baada ya kufungua mradi wa maji katika Kijiji cha Mituguru, Wilaya
ya Nachingwea mkoani Lindi. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwa
na Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo. Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu
2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze
Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” umengia katika wilaya hiyo
ambapo unatarajiwa kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Picha na Felix Mwagara.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda akizungumza na wananchi
wa Kijiji cha Ikungu, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya
kukabidhi Bajaj kwa walemavu na Pikipiki kwa watendaji wa Wilaya na Kata
mbalimbali katika wilaaya hiyo zikiwa ni kwa shughuli za maendeleo
katika Halmashauri hiyo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo
wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria
Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya”
utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya
maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akiwasalimia wapiga kura wake wa Kijiji cha Ikungu wakati wa ukimbizaji wa Mwenge wa Uhuru katika Jimbo lake la Nachingwea. Waziri Chikawe alimshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda pamoja na timu yake kwa kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake. Picha na zote na Felix Mwagara.