Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington kulia na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu, Mwakibinga leo |
KAMPUNI
ya Azam Media imetangaza kuwa tayari imeshatuma fedha kwa Bodi ya Ligi
kwa ajili ya msimu wa ligi wa Vodacom kwa mwaka 2014/ 2015.
Fedha hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema kwa timu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wao katika ligi hiyo.
Fedha hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema kwa timu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini wao katika ligi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Azam zilizopo Tazara, Dar es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema kuwa kampuni hiyo inavutiwa na aina nzuri ya ushirikiano kati yake na bodi ya Ligi.
Alisema
kuwa kupitia bodi hiyo Azam imepiga hatua kubwa katika kufanikisha
adhma yake ya kuifanya Ligi hiyo ya Vodacom kuwa ya kuvutia zaidi.
“Ligi
hii tunataka kuifanya kuwa ni moja kati ya ligi zinazovutia na kuonesha
ushindani barani Afrika, ingawaje ninajua kuwa kuna mengi ambayo
yanatakiwa kuendelea kufanywa ili kuipa nguvu zaidi ligi hii”alisema
Torrington.
Alisema
kuwa kwa kutambua hilo ndio maana Azam Media imehakikisha kuwa klabu
zote zinapata fedha mapema ili kusaidia suala zima la maandalizi.
Akizungumzia
mikakati ya baadae ya Azam Media alisema kuwa inatarajia kuanza
kuonesha soka la mitaani (street soccer) mbalimbali moja kwa moja (live)
itakayokuwa ikiendelea kwenye nchi za Kenya na Uganda.
Alisema
kuwa kwa sasa Azam Media imeanza kujikita katika nchi za Kenya, Uganda
na Malawi ambapo itakuwa ikiuza ving’amuzi vyake katika nchi hizo.
Aliongeza
kuwa pia katika kuhakikisha kuwa inatoa mwanya zaidi wa vipindi vizuri
na vya kuvutia inaendelea na vipindi vya michezo vya Morning Trumpet,
sport@8 pamoja na Kwetu House.
Kwa
upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Mr Silas Mwakibinga
alisema kuwa kwa hatua hiyo ya Azam ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha
hizo kwa wakati ni nzuri na itasaidia kuzipatia timu muda mzuri wa
kujiandaa.
Alisema
kuwa bodi yake inavutiwa sio tu na utangazaji wa vipindi unaofanywa na
Azam bali pia hata nia yao ya kuendeleza soka la Tanzania.
Azam
Media ilisaini mkataba wa miaka mitatu na wenye thamani ya TSHS
5,560,800,000 kuonesha mechi za live na za kurekodi mechi za Ligi Kuu na
fedha hizo zinalipwa kwa awamu tatu.