March 06, 2014

WAKULIMA NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO NA MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO APRIL MWAKA HUU

1Mratibu wa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo kutoka Kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, Dk.Ellen Otara-Okoedian akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusu mkutano na maeonesho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa.Kulia ni Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni John Matiko.Picha na Hussein Makame-MAELEZO. 2Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, John Matiko, akiwaeleza jambo wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa. Kulia ni Mratibu wa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo kutoka Kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, Dk.Ellen Otara-Okoedian. Picha na Hussein Makame-MAELEZO. 3Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, John Matiko (kushoto) kuhusu Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO. 4Mmoja wa wanahabari ambaye ni mpiga picha wa Televisheni ya Tumaini (katikati), akiuliza swali kwenye mkutano wa wanahabari na kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd iliyoandaa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini hapa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
………………………………………………………………………………………
Na Frank Mvungi-MAELEZO
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano na Maonesho  ya Kilimo (AGRITECH) 2014,  yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam kuanzia April 10 mwaka huu na kuwashiriksha waoneshaji wan je na ndani ya nchi katika Nyanja mbalimbali za kilimo.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa mkutano huo Dkt.Ellen Otaru- Okoedian katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Iadara ya Habari-MAELEZO leo jijini Dara es salaam.
Dkt Ellen amesema mkutano huo unalenga uwezeshaji katika kilimo ambapo wakulima wa Tanzania watapata fursa ya kukutana na wadau wakubwa wa kilimo kutoka ndani na nje ya nchi ili kujadili na kuona namna bora ya kuinua sekta ya kilimo nchini.
Alisema mkutano huo  pia utawahusisha wadau wa kilimo wakiwemo wauzaji wa pembejeo,mbolea, na madawa ya mimea, matrekta, wanaohusika na umwagiliaji, vyuo vya kilimo, biashara,  za mazao, watafiti, Taasisi za biashara za ndani na nje ya nchi, wakulima na wafugaji, Wizara zote  husika na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.
Aliongeza kuwa katika mkutano huo unaotarajiwa kuanza tarehe 10 hadi 12 aprili 2014 wakulima watapata fursa ya kuelewa umuhimu wa zana bora  za kilimo,utafiti , jinsi teknolojia ya simu za mkononi inavyoweza kubadili kilimo hapa nchini.
“Mkutano huu pia utajadili fursa mbalimbali zilizopo kwenye kilimo na mchango wa Taasisi za fedha katika kukuza kilimo hapa nchini na washiriki watapata fursa ya kujadili na kutoa mawazo yao juu ya namna bora ya kuongeza tija katika kilimo ili kupambana na janga la njaa  hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla” alisema Dk. Ellen.
Dkt. Ellen amesema mkutano huo utajumuisha washiriki toka mataifa takribani 20 yakiwemo Ujerumani, Marekani, Ufaransa, China, Japani, Kenya, Uganda na Malawi.
Naye Meneja Maonesho  na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, John Matiko alitoa wito kwa wakulima hapa nchini na wadau wote wa Sekta ya kilimo kujitokeza katika mkutano huo na pia kushiriki katika maonesho yatakayofanyika wakati wa mkutano huo.
Kwa mujibu wa Matiko, mkutano huo utakuwa na Kaulimbiu isemayo “Nguvu ya Teknolojia katika Mapinduzi ya Kilimo”.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »