BARAZA LA SANAA ZANZIBAR LATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA SUALA LA UTAMADUNI
Afisa
utamaduni Mkoa wa Kaskazini Pemba Hamad Said Mgau amelitaka Baraza la
Sanaa Zanzibar kusimamia vyema suala la utamaduni ili kudhibiti
upotoshaji wa utamaduni wa asili unaofanywa na baadhi ya wanii hapa
nchini .
Amesema
kuwa utamaduni wa asili visiwani hapa ikiwemo ngoma ya Msewe imekuwa
ikipotoshwa na baadhi ya watu kwa makusudi , hivyo ni vyema kwa Baraza
kuwa makini katika kusimamia na kulinda asili ya utamaduni huo .
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Wete , Mgau amesema kuwa
endapo Baraza halitakuwa makini kuwadhibiti watu wanaochafua utamaduni
huo , basi vizazi vijavyo vitarithi utamaduni usiolingana na maadili .
"Tunashughudia
baadhi ya wanii wanapotosha kabisa uhalisia wa ngoma ya msewe , hivyo
ni vyema Baraza la Sanaa kuwa makini na watu wa aina hiiambao
wamekusudia kuharibu uahalisia wa sanaa hiyo " alifahamisha Mgau .
Aidha
amefahamisha kwamba utamaduni wa asili
umekuwa ni kivutoa kwa watalii , na kuongeza kwamba kitendo cha
kupotoshwa kunaweza kuleta athari kwa Taifa ikiwa udhibiti wake
hautapewa kiupambele .
Hata
hivyo ameeleza kwamba Upotoshaji wa Ngoma ya Msewe zaidi umakuwa
ukifanywa na wanii nje ya Kisiwa Cha Pemba , na kusema kuwa wnaotaka
kuiga kucheza ngoma hiyo ni lazima wafuate taratibu zake .
"Msewe
asili yake ni Mombasa nchini Kenya , kwa sasa unachezwa zaidi katika
Shehia Kambini katika kijiji cha Kichokochwe lakini kama kuna msanii
anataka kuiga ifike kichokochwe na sio kupotosha kwa makusudi "
alisisitiza .
Pia
Mgau kapongeza usimamizi wa sanaa unaofanywa na kamisheni ya Utamaduni
Unguja na Pemba jambo ambalo limeongeza uhasishaji na uimarishaji wa
utamaduni Visiwani hapa .