December 31, 2013

MAJANGILI WAIBUKA UPYA , MMOJA AKAMATWA NA NYAMA YA SWALA KARIBU NA HIFADHI YA RUAHA IRINGA

Swala   wakiwa katika hifadhi 
WAKATI  taarifa ya wizara ya maliasili  na utalii iliyotolewa na naibu  waziri mwenye dhamana na  wizara  hiyo  Lazaro Nyalandu  kudai kuwa   kumekuwepo na ongezeko kubwa la ujangili wa wanyama katika hifadhi  za Taifa baada ya oparesheni ya  tokemeza ujangili kusimama ,jeshi   la  polisi mkoani Iringa  linamshikilia  mkazi mmoja  wa   kijiji  cha Idodi wilaya ya Iringa  vijijini Bw Kegete Makoga (56)  kwa  tuhuma  za  kukutwa na nyara  za  serikali ambazo ni nyama ya  swala  kilo 8 .

Kamanda  wa  polisi  wa mkoa wa Iringa  Ramadhan Mungi ameueleza  mtandao huu   leo  kuwa tukio  hilo lilitokea  Desemba 29 majira ya saa 3 usiku  katika tarafa ya Idodi  karibu na maeneo ya hifadhi ya Taifa ya  Ruaha .

 Alisema  kuwa  mtuhumiwa huyo  alikamatwa na askari  wa  hifadhi ya   Taifa ya  Ruaha Iringa ambao  walikuwa katika  doria katika  hifadhi  hiyo.

Kamanda  Mungi  aliasema   kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa na  nyama  hiyo ya Swala  baada ya doria ya askari  hao  na kwa  sasa anashikiliwa na jeshi la  polisi  kwa  uchunguzi zaidi kabla ya  kufikishwa mahakamani  kwa kosa la  kukutwa na nyara  za  serikali kinyume na utaratibu.

CHANZO:FRANCIS GODWINBLOG

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »