WANAUME wametakiwa kujenga tabia ya kucheki afya zao badala
ya kuwaachia akina mama peke yao, ikiwa ni njia ya kupambana na ugonjwa wa
Ukimwi uliozimishwa leo Dunia nzima, huku kiwilaya ya Handeni, yakifanyika
katika Kata ya Kwasunga, wilayani Handeni.
Kamanda
wa Polisi wa Wilaya Handeni, OCD Zuberi Chembera, wa pili kulia mwenye
koti jeusi akionyesha ujuzi wa kusakata rhumba katika maadhimisho ya
Siku ya Ukimwi Duniani, ambapo kiwilaya, yalifanyika Kata ya Kwasunga,
ambapoi alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu,
alihudhuria majukumu mengine ya Kitaifa. Picha zote kwa hisani ya Handeni Kwetu Blog.
Kaimu
Mkurugenzi wa Handeni, Mr Mdoe, aliyesimama, akizungumza jambo katika
madhimisho ya Ukimwi katika Kata ta Kwasunga, wilayani Handeni mkoani
Tanga.
Kamanda
wa Polisi wa Handeni, OCD Zuberi Chembera, akizungumza katika
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani, ambapo kiwilaya yalifanyika
katika Kata ya Kwasunga wilayani Handeni mkoani Tanga. Chembera
alimuwakilisha DC Muhingo Rweyemamu.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya Handeni, OCD
Zuberi Chembera, akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu,
ambapo maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wilayani hapa.
Akizungumza mbele ya wananchi waliohudhuria katika
maadhimisho hayo, OCD Chembera, alisema wanaume wengi hawapendi kupima afya
zao, hususan kujua kama wameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi, badala yake wanasubiri
matokeo ya wake zao.
Wanafunzi
katika shule ya Sekondari Kwasunga, wakiigiza mbele ya wahudhuriaji
katika Maadhimisho ya Ukimwi duniani, katika Kata yao.
Hapa wanafunzi wakiingia kwa ajili ya kuimba kwaya katika maadhimisho hayo. Hakika yalipendeza kupita kiasi.
OCD Chembera, hapa aliacha kiti na kuwasogelea kwa karibu wananchi kwa ajili ya kuzungumza nao juu ya ugonjwa Ukiwi.
Alisema inapotoke wake zao au wapenzi wao wamepata ujauzito,
hugoma kabisa kwenda kupima afya zao, jambo linaloweza kukwamisha harakati za
mapambano ya ugonjwa wa Ukimwi ndani nan je ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.
"Wanaume tuacheni tabia za kuachia akina mama waende
wakapimwe afya zao pale wanapopata ujauzito, maana hiyo si njia nzuri badala
yake wote tuwe kitu kimoja na kuyapokea matokeo hayo kwa ajili ya kulinda afya
zetu.
"Aidha ni wakati wa kila mmoja wetu kushirikiana kwa dhati
katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ambao unaendelea kuangamiza ndugu zetu,
japo kiwilaya maambukizi ya Ukimwi yanaonekana kupungua hadi asilimia 2,”
alisema.
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule
ya Msingi Kwasunga, wananchi wengi walihuudhuria sambamba na kujionea burudani
kutoka katika bendi ya Azimio pamoja na magizo kutoka kwa wanafunzi kwenye kata
hiyo ya Kwasunga.
Habari hii na picha zote ni kwa hisani ya Handeni Kwetu Blog.
EmoticonEmoticon