AGONGWA NA FUSO DARAJA LA MTO ZIGI.

December 02, 2013
Na Paskal Mbunga,Tanga..

MTU mmoja amejeruhiwa vibaya sana jana asubuhi baada ya kugongwa na gari la mizigo aina ya Fusso katika daraja la mto Zigi eneo la Amboni, nje kidogo ya jiji la Tanga.


Arif Mauji (58) mkazi wa Kibafuta wilayani hapa. 

aligongwa wakati akeendesha pikipiki kwenye daraja hilo ambapo ghafla lilitokea gari aina ya Fusso nyuma yake na kumgonga kasha kumburuta umbali wa mita 50 na kumtupa nje ya daraja na kuangukia kwenye kingo za daraja hilo akiwa taabani.


Arif aliumia sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja uso, miguu na miguu na pikipiki yake kuharibika vibaya sana kiasi cha kutoweza kutengenezwa tena.


Majeruhi alikimbizwa katika hospitali kuu ya Bombo ambako amelazwa.



Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T240 CEY ambaye alikataa katakata kutaja jina lake, alidai kuwa breki za gari hilo zilishindwa kufanya kazi na hivyo kumvamia Arif Mauji katikati ya daraja.


Hata hivyo lilipatikana jina la mmiliki wa gari hilo lililoandikwa ubavuni mwa mlango wa gari ambalo ni Daudi Mwandi wa Tarekea, Moshi.


Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Constantine Massawe amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo ambapo dereva wa lori anashikiliwa na Jeshi hilo.


 Fusso hilo lilikuwa likitokea Mombasa, Kenya.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »