WAKAZI 4737 MKOA WA TANGA WAGUNDULIKA KUWA NA MAAMBUKIZO MAPYA YA UKIMWI.

December 01, 2013



Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,Mboni Mgaza na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Benedict Ole Kuyan wakinyoosha mishumaa
kuashiria wakazi wa mkoa wa Tanga wakiungana wa wengine duniani
kuadhimisha siku ya ukimwi duniani.maadhimisho hayo kwa ngazi ya Mkoa
wa Tanga yalifanyika kijiji cha Duga Wilaya ya Mkinga.

mhandisi ushauri wa miradi ya majaribio ya barabara mkoa wa Tanga,Daniel Kemwa akipima virusi vya ukimwi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi yaliyofanyika kimkoa katika Kijiji cha Duga Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga.anayempima ni mshauri nasaha na mpimaji wa VVU  wa asasi ya Save The Society for HIV/AIDS ,Ali
Maghasa.
Burhani Yakub,Mkinga.
Jumla ya wakazi 4737 wa mkoa wa Tanga wamegundulika kupata
maambikizi mapya ya virusi vya ukimwi na 123 miongoni mwao wamekufa katika kipindi cha kuanzia januari hadi septemba mwaka huu.

Mratibu wa ukimwi Mkoa wa Tanga,Selemani Msangi alitoa taarifa hiyo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika mji mdogo wa  Duga  Wilayani.

Alisema idadi hiyo ni kwa wale waliofika kupimwa na kutibiwa katika hospitali ya Mkoa ya Bombo,Hospitali za Wilaya zote za Mkoa wa Tanga,hospitali binafsi,vituo vya afya na baadhi ya zahanati.

Tangu utaratibu wa utoaji wa dawa za kupunguza makali ya ukimwi miaka tisa iliyopita,jumla ya wagonjwa 46,808  kati yao wanaume wakiwa 14375 na wanawake 32,433 wameandikisha katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma hizo huku wanaopta dawa ni 31,102.

Akielezea changamoto zinazoikabili sekta ya afya katika kupambana na maambukizi ya ukimwi alisema vitendea kazi ni vichache hasa katika zahanati na wafanyakazi hawakidhi mahitaji.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,Katibu Tawala wa Mkoa wa
Tanga,Benedict Ole Kuyan kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Chiku Gallawa aliagiza kuimarisha utendaji wa kamati shirikishi za ukimwi katika ngazi za vijiji,mitaa,kata na Wilaya.

Aliatawaka wananchi kuacha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwabagua watu wanaoishi na maambukizi ya ukimwi ikiwa sambamba na watalaamau kwa kushirikiana na mashirika wadau kutoa elimu juu ya njia sahihi za kujikinga na maambukizi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »