Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza
maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai,
chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati
alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku
ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi
Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati alipotembelea
katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja
vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya
watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na
yeye kuzaliwa salama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya Jukwaa Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya Jukwaa Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya Jukwaa Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia
wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata
utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa
Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya
Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.
Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi
Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi moja kati ya Vitabu vya Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Mussa, baada ya ya kuzindua mpango
mkakati huo wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani,
zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi, Mashine za CD4 kwa ajili ya
Kanda za Juu Kusini, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani,
zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
Picha kwa hisani ya Sufianimafotoblog.
EmoticonEmoticon