MBUNGE wa
Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), amewataka wananchi wa Mkoa wa
Tanga kubadilika kwa kuwa na ari ya kujiletea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
Kauli hiyo
ameitoa mjini hapa leo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama cha Waandishi wa
Habari Mkoa wa Tanga (Tanga Press Club).
Alisema
kuwa ili maendeleo ya haraka yaweze kupatikana katika mkoa huo ni lazima jamii
kubadili kwa kuwa na mawazo chanya.
“Maendeleo
ni jambo muhimu sana na katika hili ni lazima tushirikiane kwa dhati.
Binafsi
ninapenda kupongeza juhudi za chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga kwa
kazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutangaza mkoa wetu.
“Nilikuwa
nasoma na sasa kila wakati tutakuwa pamoja na wanahabari pamoja na wananchi wa
mkoa wetu ili kuweza kuungana kwa pamoja katika juhudi za maendeleo za mkoa,”
alisema Mwidau
EmoticonEmoticon