NMB HAI WAIPIGA JEKI TIMU YA HALMASHAURI HIYO.

October 02, 2013
NA OMARY MLEKWA,HAI.

BENKI ya NMB  wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya mpira wa wavu ya Halmashauri ya Hai kwa ajili ya mashindano ya  timu ya Taifa  SHIMISHIMITA yanayotarajiwa kutimua vumbi  Oktoba 20 hadi Novemba 1   mwaka huu,  mkoani Dodoma.

Vifaa vilivyotolewa ni Jezi,bukta,Soks, Flana,na Traksuti vilikabidhiwa  kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ,kufuatia maombi maalumu yaliyotolewa na uongozi wa timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kufanikisha mpango wa mashindano hayo kwa timu hiyo .


Akikabidhi msaada huo ,Kwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo , Dkt Paul Chaote ,meneja wa  NMB Wilayani hapa Stella Tambikien  alisema kuwa ,NMB imetoa msaada huo kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa michezo nchini,na kwamba itaendelea kusaidia sekta hiyo ili kuboresha michezo nchini kwa kutenga sehemu ya faida inayoipata.

''NMB inaamini kwamba ili kupata wachezaji wazuri wa ngazi ya taifa ni lazima waanze kuandaliwa kwa ubora toka ngazi ya chini watakao iwakilisha taifa vyema kwenye michuano mbalimbali''alisema Tambikien

Aidha aliwaasa wachezaji hao kujituma kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanalete ushindi utakaoleta heshima kwa mkoa na kwa wale wote waliojitolea kusaidia kwa hali na mali.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi huyo pamoja na kuishukuru NMB kwa kuthamini na kuchangia michezo ,ameiomba benki hiyo kuendelea kutoa msaada , kadri inavyo pata faida ,na alitumia fulsa hiyo kuwahimiza wachezaji hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wawapo katika mashindani hayo.

‘Michezo kwa sasa ni ajira kwa hiyo nawaombeni mkajitume muweze kuuletea heshima mkoa ,na mtambue kuwa mkicheza vizuri mtapata ajira na kuwa mabalozi wazuri sehemu muendako,alisema Tambieni

Tambikieni aliyataka mabenki mengine , taasisi za fedha na wadau wa michezo nchini kuiga mfano wa NMB katika kutambua umuhimu wa kuchangia michezo ili kujenga na kuimarisha afya za wachezaji hao sanjari na kupata wachezaji bora na wenye vipaji watakao weza kuliwakailisha taifa katika michezo mbalimbali.

Aidha aliwataka wafanyakazi maofisini kujenga utaratibu wa kushiriki michezo mbalimbali ,kwani hali hiyo itasaidia kujenga afya zao na kupunguza magonjwa ya ajabu ajabu yanayo wanyemelea baadhi ya wafanyakazi ambao wengi wao wamekuwa wakinenepeana kwa kula vyakula ovyo ,hali ambayo imekuwa ikiwasababishia kuugua kila mara .

Nahodha wa  timu hiyo, Ndeakifoo Shoo alisema  kutokana na msaada huo ambao umetolewa wakati maalum wachezaji watahakikisha wanakwenda kufanya vizuri na kurudi na vikombe kama msimu uliopita.

Hata halmashauri ya Wilaya hayo inaingia katika mashindano hayo ya SHIMISHIMITA Taifa  kama mabingwa watetezi ambapo pia mwaka jana walipata walipata kombe kwa timu yenye nidhamu
 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »