DC DENDEGO AWAFUNDA WANAFUNZI WA KIKE TANGA.

October 02, 2013
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO KATIKATI KUSHOTO NI KATIBU WA CCM WILAYA YA TANGA,LUCIA MWIRU NA KULIA NI MWENYEKITI WA UWT WILAYA YA TANGA,MWANSHAMBA PASHUA WAKATI WA MAADHIMISHO YA UWT KIWILAYA AMBAYO YALIFANYIKA KATA YA PONGWE JIJINI TANGA.

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MKUU wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego amewataka wanafunzi wa kike katika shule za sekondari wilayani hapa kujitambua na kuacha kufikiria masuala ya mapenzi badala yake watilie mkazo elimu kwani ndio mkombozi wao wa maisha yao ya baadae na familia zao.

 

MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO AKIGAWA ZAWADI YA SABUNI KWA WAGONJWA KATIKA KITUO CHA AFYA PONGWE IKIWA NI WIKI YA MAADHIMISHO YA UWT AMBAPO KIWILAYA YALIYAFANYIKA KATA YA PONGWE.
Dendego alitoa kauli hiyo wakati akitoa somo maalumu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Pongwe ikiwa ni siku ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Jumuiya ya Wanawake wilaya ya Tanga(UWT) ambazo kiwilaya zilifanyika kata ya Pongwe wilayani hapa.
MGANGA MFAWIDHI WA KITUO CHA AFYA PONGWE,DR.ALLY BUGHE AKIWA AMESHIKILIA ZAWADI YA SABUNI ALIZOPATIWA NA UWT WILAYA YA TANGA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UMOJA HUO WILAYA AMBAPO YALIFANYIKA KWENYE KATA HIYO KUSHOTO KWAKE NI MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO ANAYEFUATIA NI MWENYEKITI WA UWT WILAYA YA TANGA,MWANSHAMBA PASHUA
Mkuu huyo wa wilaya aliweza kutoa somo la kuwakumbusha wanafunzi hao kuwa wazalendo wa kuipenda nchi yao ,kujitambua wao kama vijana wa kike wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupenda elimu na kuachana kufanya ngono zembe ambayo itaweza kuwapelekea kushindwa kutimiza malengo yao.

  



“Ukisoma utaheshimika na kuweza kufanya kazi yoyote kwa sababu una elimu ikiwemo kuweza kuendesha maisha yao hivyo nawasihii msome kwa bidii na mafanikio yake mtayaona “alisema DC Dendego.

 
MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO KULIA AKIMKABIDHI MGANGA MKUU WA KITUO CHAAFYA PONGWE DR.ALLY BUGHE WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UWT AMBAPO KIWILAYA YALIADHIMISHWA KATA YA PONGWE WILAYANI HAPA

MWENYEKITI WA UVCCM WILAYA YA TANGA,SALIMU PEREMBO KULIA MWANZO MEZA KUU AKIFUATILIA KWA UMAKINI VIKUNDI MBALIMBALI VYA NGOMA WAKATI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UWT WILAYA AMBAYO ILIFANYIKA KATA YA PONGWE JIJINI TANGA.
 Alisema endapo watasoma kwa bidii kwa kuzingatia yale yote watakayofundishwa darasani watapata uelewa mzuri wa kufanya vizuri katika mitihani yao na hatimaye kuweza kupata kazi nzuri ili kuweza kuzisaidia jamii zao kwa ujumla.

"Nimeunda kikosi kazi cha kuwatafuta wanafunzi wanaotoroka shuleni muda wa masomo ili kuweza kutokomeza vitendo vya wanafunzi kutoroka na hii nadhani itachochea wanafunzi kupenda masoma na kuongeza kasi ya ufaulu miongoni mwao "Alisema DC Dendego.

Aidha katika hatua nyengine mkuu huyo wa wilaya aliwataka wakina mama kujitambua kwa kuongeza jitihada zao katika shughuli za maendeleo kwani wanawake wakiwezeshwa wanaweza hivyo wahakikisha wanakuwa mstari kwa kuungana pamoja ili waweze kusonga mbele.

    “Wakina mama tupendane,tuheshimiane na tuache kukosoana badala yake tukimuona mwanamke mwenzio anakosea kaa naye umuelekeze kuliko kukosoana “Alisema DC Dendego na kusisitiza upendo kati yao.

Awali akizungumza wakati akitoa somo katika maadhimisho hayo,Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tanga, Mwanshamba Pashua aliwataka vijana wa kike wahakikishe wanatimiza ndoto zao kwa kusoma kwa bidii na kufanya kazi ili iweza kuwa msingi bora wa maisha yao.

Maadhimisho hayo yakikwenda sambamba na shughuli mbalimbali za kijamii ambapo Mkuu wa wilaya Dendego  na Katibu wa CCM wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru na viongozi wa UWT wilaya na  Kata hiyo walitembelea kituo cha Afya Pongwe kutoa zawadi kwa wakina mama wajawazito na kuwafariji wagonjwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »