MWENYEKITI WA UVCCM AWAFUNDA WAZAZI MKOANI TANGA.

September 09, 2013
NA OSCAR ASSENGA,LUSHOTO.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM)Abdi Makange amewataka wazazi na walezi mkoani Tanga kuweka msukumo wa elimu kwa watoto wao ili iweze kuja kuwa mkombozi wao katika maisha yao ya baadae.

Makange alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa mahalafi ya kumi na moja kidato cha nne ya shule ya sekondari Mlongwema ambapo alimualikisha Mbunge wa Jimbo la Lushoto,Henry Shekifu na kueleza hakuna urithi muhimu hapa nchini zaidi ya elimu hivyo wazazi wanapaswa kulitilia mkazo suala hilo kwa umakini mkubwa.

Amesema endapo wanafunzi watasoma kwa bidii ikiwemo kuzingatia masomo itawasaidia kuweza kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho na hatimaye kuweza kupata kazi nzuri ambayo itakuwa dira katika kuendeleza maisha yao na jamii zao.

  "Ukisoma utakuwa na amani ya moyo kwani unaweza unaweza kumuabudu mungu kwa moyo mmoja bila kuweka mawazo ya wapi nitapata maisha mazuri,hivyo ndugu zao naombeni msome kwa bidii na matunda yake mtayaona "Amesema Makange.

Makange pia amewataka wazazi kuwa mstari wa mbele kutoa michango muhimu inayohitajika kwa watoto wao ili iweze kuchangia kasi ya maendeleo kwenye shule hiyo.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,John Tembo amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa vya sayansi na walimu kwani yupo mwalimu mmoja tu pamoja na uhaba wa nyumba wa walimu kwani zilizopo hazitoshelezi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »