|
WANANFUNZI WAKIFUATILIA MASHINDANO YA LUGHA YA KIINGEREZA AMBAYO YALIANZA JANA KATIKA HOTEL YA REGAL NAIVERA YAKIFADHILIWA NA KINYWAJI KISICHO NA KILEVI CHA BAVARIA HOLLAND
Na Oscar Assenga,Tanga. IMEELEZWA kuwa mashindano ya Lugha yatawapa chachu wanafunzi
kutambua uwezo wao ikiwemo kutoa mwamko kwao kupenda kutumia lugha ya
kiingereza zaidi hali ambayo itapeleka kufanya vizuri katika masomo yao.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Katibu Msaidizi anayeshughulikia masuala ya
elimu Mkoa wa Tanga, Ramadhani Chomola wakati akifunga mashindano ya
lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa shule za sekondari mkoa wa Tanga
"Bavaria Malt English Competitio For Tanga Secondary 2013 yaliyojumuisha
wanafunzi zaidi ya 100 kutoka wilaya tano mkoani hapa.
Chomola
alisema mashindano hayo yatawapa mwanga mzuri washiriki kuongeza
ubunifu na bidii ya kuzungumza lugha ya kiingereza popote wanapokuwa ili
waweze kujijenga lakini pia kufahamu namna ya kuzungumza lugha hiyo.
Katika
mashindano hayo shule
ya Wasichana ya St.Christina ilifanikiwa kuwa mshindi kati ya sekondari
22 zilizoshiriki mashindano yakuzungumza lugha ya kiingereza na
kuzawadiwa seti moja ya kompyuta na printa ambapo sekondari ya
Popatlaly iliyoshika nafasi ya pili ilizawadiwa seti ya
kompyuta,Sekondari ya Rosmini iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia
runinga yenye ukubwa wa inchi 40.
Mashindano hayo ya siku mbili
yalifanyika katika viwanja vya Regal Naivera na Mkwakwani kwa udhamini
wa Bavaria Holland kupitia kampuni ya Jovet (T) limited inayosambaza
kinywaji baridi cha Bavaria Malt yalilenga kuhamasisha wananfunzi ili
waone umuhimu wa kuzungumza kingereza.
Kwa upande wake,Meneja wa
Uendeshaji Masoko wa Bavaria Holland,Rogerter Horst alisema kampuni
hiiyo inamaanini kwamba ni jambo jema kuisaidia jamii kufikia malengo
yake ya kupata maendeleo yake ya kuichumi kupitia jamii. |
|
BAADHI YA WALIMU KUTOKA SHULE MBALIMBALI MKOA WA TANGA WAKIFUATILIA MASHINDANO HAYO. |
|
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI POPATLALY NA ST.CHRISTINA WAKIWA TAYARI KWA AJILI YA MASHINDANO HAYO. |
|
MEZA YA MAJAJI WA MASHINDANO HAYO WAKIWA KWENYE MICHAKATI YAO KUHAKIKISHA KILA KITU KINAKWENDA SAWA NA BINGWA ANAPATIKANA BILA MALALAMIKIO. |
|
OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI AMBAYE ALIMUWAKILISHA MANAGING DIRECTOR JOHN KESSY KWENYE HALFA HIYO KULIA NA KUSHOTO KWAKE NI MWENYEKITI WA KAMATI YA ELIMU HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA,MUSTAPHA SELLEBOSS WAKIFUATILIA MASHINDANO HAYO. |
|
HAPA WAKITETE JAMBO. |
|
OPERATIONS MANAGER WA JOVET (T) LIMITED,CATHERINE MUNGUTI AMBAYE ALIMUWAKILISHA MANAGING DIRECTOR JOHN KESSY KWENYE HALFA HIYO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AMBAO HAWAPO PICHANI KUHUSU MASHINDANO HAYO. |
|
|
PICHA ZOTE NA PASKAL MBUNGA,TANGA.
Share this
EmoticonEmoticon