KIZIMBANI YAIADHIBU JAMHURI LIGI KUU ZANZIBAR.

September 06, 2013
Na MASANJA MABULA,ZANZIBAR.
TIMU ya soka Kizimbani Leo imeanza vema michuano ya Ligi Kuu Zanzibar baada ya kuibamiza Jamhuri mabao 2-0,katika mchezo uliochezwa dimba la soka Gombani kisiwani Pemba.

Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi kubwa ambapo Kizimbani waliweza kuandika bao lao la kwanza kupitia Othumani Mussa katika dakika ya 30 baada ya kupiga shuti kali lililomshindi lililotinga moja kwa moja wavuni.

Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi,ambapo Jamhuri iliweza kuingia uwanjani hapo kwa lengo la kusawadhisha bao hilo huku Kizimbani wakiwa na lengo la kuongeza bao hilo.

Wakionekana kujipanga na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni mithili ya mbogo aliyejeruhiwa alimanusura Jamhuri wapata bao lakini mchezaji wao alishindwa kuunganisha vizuri pasi aliyeipokea na kucheza fungo na kutoa mpira huo nje ya uwanja huo.

Kutokana na shambulio hilo,Kizimbani waliweza kuzinduka na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Jamhuri na kufanikiwa kuongeza bao lao la pili ambalo lilifungwa na Mfanyeje Mussa na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Kizimbani kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »