AFRICAN SPORTS KUWAVAA MGAMBO SHOOTING KESHO MKWAKWANI.

September 06, 2013
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
TIMU ya Mgambo Shooting kesho itashuka kwenye dimba la CCM Mkwakwani kuwavaa African Sports "Wanakimanumanu"ikiwa ni mchezo wa kirafiki utakaochukua nafasi majira ya saa kumi jioni.

Akizungumza na Tanga Raha,Ofisa Habari wa timu ya African Sports "Said Karsandas amesema maandaliiz ya kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na kila kitu kimekamilika kwa asilimia kubwa.

Karsandas alisema mchezo huo ni maalumu kwa Mgambo shooting kujiandaa na michezo yao ya ligi kuu Tanzania bara ili kuweza kufanya vema wakati African sports watatumia mchezo huo kwa ajili ya maandaliiz ya ligi ya mkoa wa Tanga.

Aidha aliwataka mashabiki na wadau wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa.


Akizungumza mechi yao inayofuata ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati yao na Ruvu Shooting,Kocha Mkuu wa Mgambo Shooting ya Tanga,Mohamed Kampira alisema maandalizi ya kuelekea mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa .

Kampira alisema matumaini yao makubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao iliyosali kwenye michuano hiyo ili kuweza kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa katika nafasi tatu za juu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »