ALIYEKUWA Mgombea Ubunge Jimbo la Muheza katika uchaguzi mkuu 2010 kupitia Chama cha United Demokratic Party (UDP),Mhina Peter amepinga kipengele cha ibara ya 117 cha kwanza katika rasimu ya katiba kinachoeleza sifa za mgombea ubunge,kuwa awe na umri usiopungua miaka 25 kwa sababu suala hilo linawanyima fuksa wa watanzania.
Mhina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Tanga alisema yeye alisema mtu anaweza kugombea ubunge akiwa na miaka kuanzia 18 kwa sababu ndio umri wa kijana unapokuwa ukianzia hivyo wataweza kuwapa maendeleo wananchi wao wanaowaongoza.
Alisema suala jengine ambalo anapingana nalo kwenye kipengele 1b katika rasimu ya katiba kinachosema mtu anayetaka kugombea ubunge awe anajua kuongeza na kuandika kiswahili na kingereza akiwa tayari ameshamaliza kidato cha nne.
Aidha alisema kuna watu ambao wanafika darasa la nne na kwa sababu wanauelewa mzuri wa kuongeza wapewe nafasi katika kugombea nafasi kama hiyo ili kuweza kuwatumikia wananchi wake bila kuwepo kwa vikazo hivyo.
Alisema hata hivyo misingi ya hilo baraza lenyewe la katiba haikuzingatia elimu kwa sababu wapo watu walioingia kwenye mabaraza hayo hawakusoma kabisa zaidi ya kuwa na uelewa wa mkubwa wa kutafakari mambo.
"Tunaweza kuzingatia misingi ya elimu kwa madaktari,wahandisi lakini kwenye suala la ubunge taaluma yake kubwa ni utendaji tu na sio vyenginevyo "Alisema Mhina.
EmoticonEmoticon