(Mmiliki wa Kampuni ya Kokoliko Disgner Mama Sophia akiwa katika pozi)
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
Kampuni ya disgner ya Kokoliko ilinayomilikiwa na Mama Sophia Production imeelezea malengo yake ya kuendelea kuwabunia mavazi wabunifu mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kutangaza utamaduni wetu wa Africa.
Sophia ambaye alibuni vazi la washiriki walioingia kwenye fainali za Miss Utalii mwaka 2013 ambalo mwaka huu lilifanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani kuanzia hatua ya mwanzo mpaka mwisho.
Alisema baada ya shindano hilo kumalizika ukumbini miss Utalii namba nne ambaye alipata nafasi ya kwenda kushiriki Mashindano ya Miss Kossovo na kufanikiwa kushika nafasi ya nne na baadaye kurejea mkoani hapa na kupokewa kushujaa na umati wa wakazi wa Tanga wakiongozwa na mama Sophia Production.
Baada ya mrembo huyo kutua mkoani hapa alifanyiwa sherehe katika Hotel ya CBA iliyopo Raskazone jijini Tanga ambayo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali mkoani hapa ambayo ilianza saa tatu usiku na usiku ambapo mrembo huyo alipata nafasi ya kuwashukuru wakazi wa Tanga akiwemo Mama Sophia Production kwa kumsapoti.
Aidha Mama Sophia anasema filamu yake mpya ya Tanga Line ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni anaimani itafanya vizuri kwenye tasnia ambayo imejaa maadili ya kipwani na kimwambao iliyo na maadili ya kimwambao.
Filamu hiyo imeandaliwa na Kampuni maalumu ya filamu hapa nchini na kampuni ya Sophia Production na endapo kama unataka maelezo zaidi kuhusu filamu hiyo wasiliana nao 0713510530.
Mwisho.
EmoticonEmoticon