Simba na Mgambo kupambana leo uwanja wa Taifa kuwania pointi tatu.

May 08, 2013
Kikosi cha timu ya Mgambo Shooting ambacho kitapambana na Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.

KOCHA Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting ya Tanga,Mohamed Kampira amesema timu yao imapania kupata matokeo mazuri katika mechi yao ya Ligi kuu Tanzania Bara dhidi yao na Simba itakayochezwa leo saa kumi jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kampira alisema kikosi ambacho kitashuka kwenye dimba hilo hii leo kitakuwa chenye upinzani mkubwa kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kuelekea mechi hiyo .

Alisema licha ya kujiandaa kwa mechi hiyo lakini pia wao wamejiandaa katika mechi zao zilizosalia ili kuhakikisha wanachukua pointi tatu muhimu kwani lengo lao ni kumaliza ligi hiyo wakiwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo.

Blog hii inaitakia kilala heri Mgambo shooting kwenye mechi hiyo ili iweza kufanya vizuri kwani tunaamini uwezo wanao na nia pia wanayo hivyo wachezaji wahakikisha wanacheza kwa umakini mkubwa sana.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »