Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa vinatakiwa kuendelea
na mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoshirikisha watoto wenye umri chini ya
miaka 15 katika ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa na fedha za uendeshaji
kutoka kwa mdhamini.
Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap),
mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika
ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata.
Hivyo, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake (vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na mashindano wakati suala la vifaa
na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa mdhamini wa mashindano.
Vifaa na fedha zitapatikana wakati wowote baada ya
taratibu husika kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka
nje ya Tanzania.
Ni matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashindano mazuri
mwaka huu kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni ya Coca Cola ilianza kudhamini
mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa yakifanyika kila
mwaka.
Mwisho.
EmoticonEmoticon