RAIS DK. MWINYI KUSHIRIKI SHEREHE ZA MIAKA 50 YA SIKU YA USHINDI MSUMBIJI

September 07, 2024

 




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili jijini Maputo, Msumbiji akitokea Indonesia na kupokewa kwa gwaride maalum na ujumbe wake akiwemo Mkewe Mama Mariam Mwinyi.

Katika uwanja wa ndege wa Maputo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji akiwemo Waziri wa Afya wa nchi hiyo.

Rais Dk. Mwinyi atashiriki Sherehe za Miaka 50 ya Siku ya Ushindi nchini Msumbiji.

Kuhudhuria kwake katika sherehe hizo kunatokana na mualiko Maalum kutoka kwa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi.

📅 07 Septemba 2024 📍Maputo, Msumbiji




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »