WAFADHILI WATOA FEDHA KWA AJILI YA UTEKELEZAJI MRADI WA KUFUA UMEME KAKONO

April 10, 2024

 Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma


Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana Shirika la Maendeleo la Ufaransa wamesaini mkataba ambapo kiasi cha Euro Millioni 110 kitatolewa na shirika hilo na Benki ya maendeleo ya Maendeleo ya Afrika itatoa Dolla Million 161 na umoja wa Ulaya utatoa Euro millioni 134 kwa ajili ya Mradi wa kuzalisha umeme wa Kakono.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu El- maamry Mwamba ambaye ameshukuru wafadhili wote wa tatu Kwa michango yao muhimu ambayo itasaidia kupatikana fedha kwa ajli ya mradi huo muhimu.

Mradi wa kufua umeme wa Kakono unaendana na mpango wa maendeleo wa Taifa ambao unamaudhui ya kujenga uchumi shindani na viwanda kwa ajili ya maendeleo ya watu kupitia uboreshaji wa miundo mbinu na upatikanaji wa nishati ya uhakika na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji wa mifumo ya elimu na ujuzi, amesema.

“Nifuraha kuona kwamba Sekta ya nishati ni moja ya mradi wa kipaumbele kwa Shirika la Maendeleo la Ufaransa pamoja na umoja wa Ulaya,” alibainisha Dkt, Natu

Aidha mpango wa Nishati wa Umeme wa Kakono unaendana na Mkakati wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mwaka 2021-2025 ambavyo kati ya vipaumbele vyake vya kiuendeshaji ni pamoja na sekta nishati .

Ameongeza kusema ujenzi wa mradi huo utasaidia Kuongeza uzalishaji wa umeme nafuu kwa nguvu za maji kukabiliana na upungufu wa umeme katika gridi ya Taifa kwa maeneo ya kusini magharibi mwa Tanzania.

“Ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa Kakono utakuwa Mbadala wa Mitambo ya kufua umeme kwa mafuta ambayo hutumika kuongeza uzalishaji wa umeme kwenye gridi ya taifa ili kupunguza mgao,” alibainisha

Imeelezwa kwamba Utekelezaji wa mradi huu unaoendelea na utakamailika mwaka 2026 na kukabidhiwa kwa serikali mwaka 2028, mradi unatarajia kuongeza megawati 87.8 kwenye gridi ya taifa pindi utakapokamilika.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt James Mataragio amesema miradi inayofadhiliwa ni pamoja na Mradi wa kuongeza usambazaji kwenye Gridi (Upgrade Transmission Grade) Mradi wa kuzalisha megawati 150 wa jua Kishapu, kuna mradi mwingine unaohusisha Tanzania na Zambia (Tanzania Zambia Interconnection) Mradi wa umeme wa jua Mafia ambao utazalisha megawati 5.

“Sisi kama Serikali tunawashukuru sana kwa kuendelea kutoa ufadhili katika hii miradi kwa sababu licha ya kusaidia ujenzi wa miradi wamekuwa wakitoa msaada wa kiufundi,” alibanisha.

Dkt, Mataragio amesema Serikali itahakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – Maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert wakipongezana baada ya kusaini mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – Maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert, wakionesha mikataba ya Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, baada ya hafla ya kusaini mikataba hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini, Bi. Celine Robert, wakisaini mikataba ya Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Baadhi ya wawakilishi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati wakifuatilia kwa karibu hotuba mbalimbali zilizotolewa katika hafla ya utiaji saini wa Euro milioni 34.86 sawa na shilingi bilioni 96.47 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa nguvu za maji wa Kakono, katika hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »